

Zaidi ya Lebo: Kuelewa na Kulea Watoto Wenye Autism na ADHD
Autism na ADHD ni miongoni mwa hali ambazo bado zinaeleweka vibaya — zikizungukwa na hofu, uvumi, na mara nyingine lawama. Katika kikao hiki cha moja kwa moja, Hussein Mshunga, mwanasaikolojia wa watoto na mtaalamu wa autism na ADHD, atatusaidia kuzielewa kwa uwazi: dalili za kuziona, jinsi utambuzi unavyofanyika hapa nchini, na jinsi zinavyoathiri makuzi ya mtoto. Grace Mwasi ataongeza upande wa malezi ya vitendo — jinsi ya kumlea na kumtetea mtoto nyumbani, shuleni na katika jamii.
Ni kwa ajili ya wazazi, walezi, walimu, watoa huduma za afya, na yeyote anayemjali mtoto.
Una swali? Karibu — kutakuwa na kipindi cha maswali na majibu, na unaweza kutuma swali lako mapema wakati wa usajili.
Jiunge nasi Jumamosi, tarehe 22 Agosti 2026, saa 12 jioni hadi saa 1 usiku.